BODA WAANGUKIWA NA MASHARTI MAGUMU
Wahudumu wa boda boda watahitaji usajili mpya unaoonyesha maeneo wanakohudumu, sare tofauti kulingana na kaunti ndogo wanazotoka miongoni mwa masharti mengine katika juhudi za kuidhibiti sekta hiyo ambayo imedhaniwa kuwa maficho ya wahalifu.
Katika mkutano wa washikadau, iliafikiwa kwamba kila anayesajiliwa atahitajika kuwa na leseni ya uendeshaji wa magari, cheti cha tabia njema miongoni mwa mahitaji mengine.
Aidha, mwenyekiti wa kila kituo atawajibikia tukio la uvunjaji sheria na mwanachama wake.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 


























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































