#Business

KRA YALENGA KUKUSANYA KSH 300B KUTOKA KWA WALIPA KODI MILIONI 11

Mamlaka ya kukusanya Ushuru nchini (KRA) inalenga kukusanya zaidi ya shilingi bilioni 300 kutoka kwa walipa kodi wa sekta isiyo rasmi milioni 11 katika mwaka huu wa kifedha.

Kupitia Idara yake ya Walipakodi wa kadri na Wadogo (MST), KRA inarahisisha michakato ya ushuru kwa Biashara Ndogo na za Kati (MSMEs) ili kuongeza uzingatiaji na mapato.

Kamishna George Obell amebainisha kuwa biashara ndogo ndogo na za kati huchangia asilimia 40% hadi 50% ya Pato la Taifa na huajiri wafanyakazi wengi lakini wanakabiliwa na changamoto kama vile taratibu ngumu za kodi na usaidizi mdogo. Kufuatia hilo, KRA inapanga kufungua zaidi ya vituo 10,000 vya mawakala ili kukamilisha ofisi zake 136, kuzindua kampeni za elimu ya kodi, na kutoa motisha kwa biashara zinazotii sheria hizo.

Vile vile KRA itatoa zana za kidijitali na kufanya kazi na wahusika wa sekta hiyo ili kuleta suluhisho mahususi ya sekta ambayo inahimiza utiifu wa kodi kwa hiari.

Imetayarishwa na Maurine Amwayi

KRA YALENGA KUKUSANYA KSH 300B KUTOKA KWA WALIPA KODI MILIONI 11

JUMA APONGEZA RISING STARLETS

KRA YALENGA KUKUSANYA KSH 300B KUTOKA KWA WALIPA KODI MILIONI 11

WANAFUNZI WA LITEIN WARUDISHWA NYUMBANI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *