#Local News #uncategorized

KEBS, UPINZANI WATOFAUTIANA KUHUSU SUKARI

Shirika la kutathmini ubora wa bidhaa nchini KEBS limepuzilia mbali madai kwamba sukari isiyofaa kwa matumizi ya kinyumbani inayosambazwa nchini jinsi ilivyoibuliwa na mrengo wa upinzani.

Katika taarifa rasmi, KEBS imesema madai hayo hayana ukweli, na kusisitiza kuwa sukari yote inayoazalishwa nchini na inayoagizwa hufanyiwa tathimini ya kina kabla ya kuruhusiwa sokoni.

Hii ni baada ya upinzani kuibua mdai kwamba kuna shehena ya tani 2,500 ambayo haifai kutumiwa na binadamu ila imeingizwa nchini.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

KEBS, UPINZANI WATOFAUTIANA KUHUSU SUKARI

TAARIFA YA EAC KUHUSU TAHARUKI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *