SHIKANGWA AONDOKA SIMA QUEENS
MSHAMBULIAJI wa Harambee Starlets, Jentrix Shikangwa ameondoka rasmi Simba Queens, na hivyo kuashiria mwisho ukurasa mzuri katika soka la wanawake Tanzania. Tangazo hilo limekuja ikiwa ni sehemu ya kile kinachoonekana kuwa ni mabadiliko makubwa ya kikosi kilichofanywa na wababe hao wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania.
Shikangwa alijiunga na Simba Queens Januari 2024 baada ya kusaini mkataba mfupi wa miezi sita na timu ya Asia, Beijing Professional ya nchini China, na kuacha historia nzuri. Msimu wa 2024-25, alikuwa mfungaji bora wa klabu hiyo, akifunga mabao 24 na kuisaidia Simba Queens kumaliza kama washindi wa pili wa ligi.
Mchango wake katika soka la Tanzania umekuwa wa kipekee. Msimu wa 2022-23, Shikangwa alitwaa Kiatu cha Dhahabu cha Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania, akifunga mabao 17 na kudhihirisha ubabe wake kama mmoja wa washambuliaji bora wa Afrika Mashariki.
Imetayarishwa na Nelson Andati
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































