MJELEDI WA SHA WAANGUSHWA
Waziri wa afya Aden Duale amesema kuwa madaktari 12 wanachunguzwa kuhusiana na madai ya kuhusika katika ulaghai kupitia bima ya afya ya SHA.
Katika kikao na wanahabari, Duale amesema kuwa madaktari hao walitoa maelezo ya wagonjwa hewa ili kuilaghai bima hiyo ya afya.
Madaktari hao aidha wamepokonywa leseni ya kuhudumu na kesi hiyo imewasilishwa kwa idara ya uchunguzi wa jinai DCI kwa uchunguzi zaidi.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 


















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































