KARUA ASEMA ATAONGOZA KWA MUHULA MMOJA PEKEE
Kiongozi wa Chama cha People’s Liberation Party (PLP), Martha Karua, ametangaza rasmi azma yake ya kuwania urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2027 akiahidi kwamba endapo atachaguliwa, atahudumu kwa muhula mmoja pekee.
Akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Kitaifa wa chama hicho, Karua amesema uamuzi wake haujatokana na tamaa binafsi, bali ni kutokana na dhamira ya dhati ya kuhudumia umma na kurejesha imani ya Wakenya kwa taasisi za kidemokrasia.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































