#uncategorized

STARS UWANJANI KUWEKA HISTORIA

Kwa mara ya kwanza baada ya miaka 38, Harambee Stars itafuzu katika awamu ya muondoano ya mashindano makubwa ya bara, watakapomenyana na aMadagascar katika awamu ya robo fainali ya mashindano ya mataifa bibngwa barani Afrika jkwa wachezaji wa ligi za nyumbani CHAN hii leo.

Wapinzani wao Madagaska wana uzoefu katika jukwaa la bara hili, wakitinga nusu fainali  ya mashindano hayo mwaka 2022 nchini Algeria kabla ya kumaliza katika nafasi ya 3.

Mechi hiyo iliyosubiriwa kwa hamu, itaandaliwa katika uwanja wa Kasarani jijini Nairobi majira ya saa kumi na moja jioni.

Katika mechi nyingine ya awamu hiyo, majirani Tanzania watashuka dimbani dhidi ya mabingwa mara 2 Morocco, waliomaliza nafasi ya pili nyuma ya Kenya katika awamu ya makundi.

Mechi hiyo pia itaandaliwa saa kumi na moja nchini Tanzania.

Imetayarishwa na Nelson Andati

STARS UWANJANI KUWEKA HISTORIA

MAREJEO YA FUJO

STARS UWANJANI KUWEKA HISTORIA

RFC WALENGA KUREJESHA TAJI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *