#Sports

POLICE FC, NAIROBI UNITED WAFAIDI MABAO YA UGENINI

Klabu ya Police FC inayoshiriki ligi kuu ya soka nchini KPL imejipatia nafasi katika awamu ya 2 ya mwondoano kwenye mashindano ya kuwania ubingwa wa klabu bingwa barani Afrika, licha ya kichapo cha mabao 2:0 mikononi mwa Mogadishu City.

Police walifuzu kwa faida ya bao la ugenini kufuatia ushindi wa mabao 3:1 katika mkondo wa kwanza.

Police FC watakabana koo na Al-Hilal wa Sudan katika awamu ya pili, mkondo wa kwanza ukiratibiwa tarehe 17 Oktoba.

Kwingineko, Nairobi United pia watamenyana na Etoiles Sportive du Sahel katika awamu nya 2 ya mwondoano katika mashindano ya CAF Confederations licha ya sare ya mabao 2 na sare ya bao 1 dhidi ya NEC FC ua Uganda katika awamu ya kwanza.

Naibois wameingia awamu hiyo kwa faida ya mabao vili vile.

Imetayarishwa na Nelson Andati

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *