POLISI WACHUNGUZA MAUAJI YA TALANTA
Polisi katika eneo la Nairobi area wanaendesha uchunguzi kubaini kiini cha kifo cha mfanyakazi wa ujenzi katika uwanja wa michezo wa Talanta ambaye mwili wake ulipatikana uwanjani humo Jumamosi asubuhi na wajenzi wenzake.
Mwili wa Sammy Kyengo mwenye umri wa miaka 35, uligunduliwa kwenye kidimbwi cha maji wiki moja baada ya mkewe kuripoti kutoweka kwake.
Kulingana na familia, mwendazake alikuwa akilalamikia kutolipwa na mwanakandarasi anayejenga uwanja huo tangu mwezi Julai mwaka huu, na alikuwa amepanga kuiacha kazi hiyo pindi atakapolipwa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 


























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































