WANAOTOZA P3 WAKAMATWE, VIONGOZI
Viongozi nchini wamependekeza kukamatwa kwa maafisa wanaowatoza fedha wakenya walio na malalamishi ya kudhulumiwa kabla ya kuwapa fomu za P3, wakisema fedha hizo zinatozwa kinyume na sheria.
Akizungumza katika kongamano la ugatuzi, gavana wa Elgeyo Marakwet Wesley Rotich, amesema matozo hayo yamechangia kuongezeka kwa visa vya dhuluma hasa vya kijinsia, waathiriwa wakikosa fedha za kulipia fomu hizo.
Kauli yake imesisitizwa na kaimu afisa mkuu wa baraza linalozuia magonjwa ambukizi Douglas Bosire.
Imetayarishwa na Nelson Andati
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































