OPERESHENI MAALUM YAAGIZWA JIJINI
Hali ya kawaida inatarajiwa kurejea katikati mwa jiji la Nairobi baada ya Waziri wa usalama wa kitaifa Kipchumba Murkomen kuagiza operesheni maalum kwa lengo la kukabili magenge ya uhalifu ambayo yameibua hofu jijini.
Kulingana na Murkomen, wengi wa washukiwa hujifanya Watoto wa kurandaranda mitaani ambao baadaye huwashambulia wapita njia na wafanyabiashara na kuwaibia.
Wakenya wametaja maeneo ya Kimathi Street, Moi Avenue na Mbotela Stretch iliyoko kwenye barabara ya Jogoo kuwa hatari zaidi.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































