WAKENYA WALIOHUKUMIWA KIFO UGHAIBUNI KUREJESHWA, SERIKALI
Serikali imeimarisha juhudi za kuwarejesha nchini wakenya wasiopongua 1,000 wanaokabiliwa na hukumu ya kifo katika mataifa mbali mbali.
Haya ni kwa mujibu wa mkuu wa mawaziri Musalia Mudavadi, akizungumza baada ya kukutana rasmi na Stephen Munyakho, aliyerejea nchini baada ya kuponea hukumu ya kunyongwa nchini Saudi Arabia.
Mudavadi amekiri kuwepo kwa changamoto kuwarejesha nchini wakenya hao ila akasisitiza kuwa serikali inajitahidi.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































