KAMATI YA AFYA YAFIKA ELDORET KUCHUNGUZA BIASHARA YA FIGO
Kamati ya bunge kuhusu afya imezuru mji wa Eldoret kaunti ya Uasin Gishu kufanya uchunguzi katika madai ya kuendeshwa kwa biashara ya kuuza figo vinavyohusisha vijana wengi.
Kamati hiyo imezuru Eldoret baada ya mbunge wa Nandi Hills Benard Kitur kuwasilisha hoja bungeni akisema vijana wengi wameathirika baada ya kuuza figo zao.
Tayari watu wanaodaiwa kuuza figo zao wamewasili kutoa maelezo yao kwa kamati hiyo kuhusu yaliyojiri japo kwa njia ya siri.
Kamati maalum iliyobuniwa na Waziri wa afya kuendesha uchunguzi huo ilikamilisha kibarua chake na kuwasilisha na kuwasilisha ripoti yake kwa Waziri Adan Duale.
Imetayarishwa na Maureen Mukhobe
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































