#Sports

MALKIA MBIONI KUREJESHA MATUMAINI

Timu ya taifa ya voliboli ya akina dada Malkia Strikers wamenajiandaa kuweka hai matumaini yao kuendelea katika awamu zaidi kwenye mashinandano ya ubingwa wa mataifa nchini Thailand watakapomenyana na Ponda hii leo saa kumi unusu katika raundi ya 2.

Hii ni baada ya kupoteza kwenye raundi ya 1 kwanza dhidi ya Ujerumani kwa seti 3:0 Jumamosi katika kundi G.

Akizungumza baada ya mazoezi yao hapo jana, mkufunzi mkuu wa timu hiyo Geoffrey Omondi, amesema timu hiyo ina uwezo wa kuwakalifisha Poland ambao wanashikilia nafasi ya 3 katika jedwali la shirikisho la Voliboli Ulimwenguni FIVB.

Kabla ya mashindano hayo, Kenya ilipoteza mikononi mwa Spain na Vietnam katika mechi za kirafiki wiki jana, na watacheza dhidi ya Vietnam katika raundi ya 3 na ya mwisho ya makundi Jumatano.

Wakati uo huo, nahonda wa timu hiyo Meldina Sande, amethibitisha kuwa baadhi ay wachezaji wamepokea marupurupu yao baada ya malalamishi.

Imetayarishwa na Nelson Andati

MALKIA MBIONI KUREJESHA MATUMAINI

WAANDALIZI KUIONEA CHAN KWENYE RUNINGA

MALKIA MBIONI KUREJESHA MATUMAINI

KENYA YAPTA HOLIDEI MPYA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *