#Local News

WASHUKIWA 2 WAPIGWA RISASI MATHARE

Washukiwa 2 wa wizi wa kimabavu walipigwa risasi na polisi katika mtaa wa Mathare hapa Nairobi.

Polisi wanasema wawili hao walitumia vurugu zilizotokea kwenye barabara ya Outer ring kuwapora watu waliokuwa wakitembea kwa miguu kwenye barabara ya Juja.

Vifaa mbali mbali vya wizi vilipatikana kutoka kwa washukiwa hao huku mmoja akifanikiwa kutoroka.

Imetayarishwa na Maureen Mukhobe

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *