#Local News

WANGAMATI AAGIZWA KUKAMATWA

Aliyekuwa gavana wa Bungoma Wycliffe Wangamati na mbunge wa Webuye West Dan Wanyama, wamepata pigo baada ya mkurugenzi wa mashtaka ya umma DPP kuidhinisha kwamba wafunguliwe mashtaka ya ufisadi unaohusisha ufujaji wa shilingi milioni 70.2.

Fedha hizo zinaripotiwa kufujwa kupitia utoaji wa kandarasi kwa kampuni zilizo na uhusiano wa karibu na wawili hao ambao sasa DPP ameagiza wakamatwe Pamoja na washirika kadhaa akiwemo Nicholas Wangamati, Michael Wangamati, Edward Makhanu na Sandra Soita.

Mwingine ambaye pia mashtaka ya ufisadi yameidhinishwa dhidi yake ni gavana wa Bomet Hillary Barchok na maafisa kadhaa wa kaunti hiyo.

Imetayarishwa na Nelson Andati

WANGAMATI AAGIZWA KUKAMATWA

SIKU YA GAVANA MUTAI SENETI

WANGAMATI AAGIZWA KUKAMATWA

WAKENYA WAFAGIA JUKWA LA USHINDI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *