WAUGUZI WASITISHA MGOMO TRANS NZOIA
Huduma za matibabu katika hospitali za umma kaunti ya Trans Nzoia zinatarajiwa kurejelea hali ya kawaida hii leo kufuatia kusitishwa kwa mgomo wa wauguzi ambao umedumu kwa zaidi ya mwezi mmoja.
Hatua hiyo imejiri kufuatia mazungumzo ya kina kati ya muungano wa wauguzi KNUN na serikali ya kaunti hiyo, KNUN ikiongozwa na katibu mkuu tawi hilo Edward Cheruiyot ikisema mwajiri wao amekubali kutekeleza matakwa yao kikamilifu.
Aidha, Cheruiyot amesema muungano huo utafuatilia utekelezaji wa makubaliano hayo ili kuhakikisha wanachama wanasaidika wanapowahudumia wagonjwa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 






































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































