#Sports

HOJLUND KUJIUNGA NA NAPOLI

Napoli siku ya Jumatatu ilitangaza kumsajili Rasmus Hojlund kwa mkopo kutoka Manchester United akiwa na jukumu la kumnunua, na hivyo kumaliza kipindi kigumu cha mshambuliaji huyo Old Trafford.

Vyombo vya habari vya Uingereza viliripoti kwamba Napoli italipa pauni milioni 38 ($51.5 milioni) kwa mkataba wa kudumu kwa Hojlund msimu ujao wa joto.

Raia huyu wa denmark mwenye umri wa miaka 22 alisajiliwa na United kutoka Atalanta miaka miwili iliyopita lakini alitatizika kukidhi bei yake ya pauni milioni 64 katika timu ambayo haikufanya vizuri.

Hojlund alitatizika katika ligi kuu ya Uingereza msimu uliopita, akifunga mabao manne pekee katika michezo 32, lakini alifunga mara sita katika harakati za United kufika fainali ya Ligi ya Europa.

Napoli walikuwa wakihitaji mshambuliaji mpya baada ya Romelu Lukaku kupata jeraha la paja kabla ya kuanza kwa msimu mpya, huku vyombo vya habari vya Italia vikiripoti kuwa anaweza kuwa nje ya uwanja hadi 2026.

Hapo awali Hojlund aliichezea Atalanta nchini Italia, akifunga mabao 10 katika mechi 34 alizocheza.

Napoli ya Antonio Conte ilishinda Scudetto kwa pointi moja mbele ya Inter Milan msimu uliopita.

Napoli wameanza vyema ulinzi wao wa kutetea taji, wakishinda mechi zao mbili za mwanzo huku mchezaji aliyesajiliwa majira ya kiangazi Kevin De Bruyne akivutia.

Imetayarishwa na Nelson Andati

HOJLUND KUJIUNGA NA NAPOLI

MASHINDANO YA GOFU YASHIKA KASI

HOJLUND KUJIUNGA NA NAPOLI

ASENSIO AJIUNGA NA FENERBAHCE

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *