KIZINGITI KWENYE UCHUNGUZI WA MAUAJI YA WAKILI
Ukosefu wa kamera za CCTV kwenye barabara ya Magadi jijini Nairobi ndicho kizingiti kinachochelewesha kukamatwa kwa washukiwa wa mauaji ya wakili Kyalo Mbobu aliyeuawa kwa risasi wiki jana.
Haya ni kwa mujibu wa Waziri wa usalama wa kitaifa Kipchumba Murkomen, hasa baada ya wakenya kulalamikia kucheleweshwa huku ikilinganishwa na uchunguzi katika mauaji ya aliyekuwa mbunge wa Kasipul Ong’ondo Were.
Ibada ya wafu ya wakili huyo imeratibiwa leo huku akitarajiwa kuzikwa Jumatano nyumbani kwake.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 


























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































