KRA YAOKOA MAMILIONI YA FEDHA MOMBASA
Mamlaka ya ya ukusanyaji wa ushuru nchini KRA imezuia jaribio la kulaghai serikali zaidi ya shilingi milioni 123 za kodi kupitia uidhinishaji usiofaa wa Konteina 161 ya mchele katika kituo cha Konteina cha Mombasa.
Kupitia taarifa, KRA imesema kuwa ulaghai huo uliofanyika kati ya tarehe 1 na 23 Agosti mwaka huu ulitambulika wiki jana baada ya ukaguzi ambao huratibiwa na kwamba uchunguzi zaidi unaendelea kuhusiana na kisa hicho.
Aidha mamlaka hiyo imehakikisha kuwa inashirikiana na tume ya maadili na kukabili ufisadi EACC pamoja na wadau wengine ili kuhakikisha wahusika wamekamatwa.
Imetayarishwa na Maureen Amwayi
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































