WADAU WAZUNGUMZIA DYSLEXIA
Serikali za mataifa ya bara Afrika zimehimizwa kuwekeza katika vifaa vinavyowezesha kusoma watoto walio na changamoto za kusoma na kuandika yaani dyslexia, ili kuwawezesha kuafikia viwango vya juu vya masomo sawa na watoto wasio na changamoto hizo.
Ni wito ambao umetolewa na washikadau katika sekta ya masomo, wakiwemo viongozi, wanaobuni sera na wazazi wa watoto walio na changamoto hizo walipokutana kwenye kongamano la kwanza la kutoa hamasa kuhusu changamoto hizo za dyslexia.
Aidha, serikali hizo zimehimizwa kuwapa walimu wa chekechea uwezo wa kutambua matatizo hayo miongoni mwa watoto.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































