MASHARTI MAPYA KWA WAKOPAJI WALIO NA REKODI MBOVU
Wakenya walio na rekodi mbovu ya madeni katika benki mbali mbali nchini huenda wakumbana na masharti magumu wakati wa kuchukua mikopo huku benki zikitarajiwa kuanza kutumia masharti hayo yaliyoegemezwa kwa kiwango rejea cha kifedha KESONIA katika utoaji wa mikopo.
Kulingana na gavana wa benki kuu ya Kenya Kamau Thugge, hatua hiyo hailengi kumtenga yeyote katika mfumo rasmi wa mikopo ila wakopaji hao watatakiwa kuridhika na mfumo huo wa gharama kubwa ya mikopo tofauti na wengine kama njia ya kuhakikisha kuna uwazi.
Mpango huo ni tofauti na uliowekwa mwaka 2019 ambao ulihitaji stakabadhi za mkopaji kuidhinishwa na benki kuu, ila sasa wakopaji wataidhinishwa na bodi ya benki binafsi.
Kwa upande mwingine benki zitahitajika kuwasilisha kiwango cha riba wanachotoza na riba wanayotoza kila mwezi kwa wakopaji kama njia ya kuhakikisha benki zinafuata masharti hayo.
Benki zinatarajiwa kuanza kutumia mfumo huo ndani ya miezi 3 huku zikianza kutozwa kulingana na mpango huo mpya kuanzia tarehe 1 Disemba.
Imetayarishwa na Maureen Amwayi
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































