FAMILIA KILIFI YALILIA HAKI KWA MWANAO
Familia moja katika kaunti ya Kilifi inataka haki itendeke kwa binti
yao mwenye umri wa miaka 15 aliyeaga dunia baada ya kudaiwa kupigwa na mwalimu
mmoja wa shule ya msingi ya Gongoni.
Kutokana na upasuaji wa maiti, ripoti ilibaini kwamba Anestine Tunje wa
gredi ya 8 alifariki kutokana na uvujaji damu wa ndani wa kichwa.
Aidha, familia ya Anestine inaamini kwamba majereha ambayo binti yao
alipata ni kutokana na adhabu ya kimwili aliyoipata shuleni humo.
Kanja: tutahakikisha uwazi katika usajili
Inspekta jenerali wa polisi Douglas Kanja amewaagiza maafisa watakaosimamia
zoezi la usajili wa makurutu kuhakikishia kuwa zoezi hilo
linafanywa kwa uadilifu ili kuiimarisha imani ya umma katika huduma
ya kitaifa ya polisi NPS.
Zoezi hilo linatarajiwa kuanza rasmi tarehe tatu hadi tarehe 9 mwezi
huu na linalenga kuwapata makurutu 10,000.
Aidha, Kanja amesema kuwa zoezi hilo linafuatiliwa na mashirika
mbalimbali ili kuafikia viwango vinavyotakiwa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 


























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































