FAIDA ZA EGP ZAWEKWA WAZI
Kenya inatarajiwa kuokoa zaidi ya shilingi bilioni 150 kila mwaka iwapo mfumo wa kielekroniki wa kufanya uagizaji unaotarajiwa kuanza kutumika kuanzia Julai 1 mwaka ujao utatekelezwa.
Mfumo huo ambao utagharimu shilingi bilioni 5 utashirikiana na benki kuu ya dunia na shirika la fedha la kimataifa IMF katika kusimamia uagizaji ili kurahisisha shughuli hiyo, kuhakikisha kuwa kuna uwazi, kupunguza visa vya ufisadi miongoni mwa mengine.
Kulingana na tume ya maadili na kukabili ufisadi EACC, shilingi bilioni 2 hupotea kila siku kupitia mfumo wa sasa wa uagizaji huku jumla ya shilingi bilioni 600 zikipotea kila mwaka ambapo asilimia 70 ya pesa hizo hupotea kupitia uagizaji.
Imetayarishwa na Maureen Amwayi
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































