BALAA YA DHARURA AMREF
Madaktari walioangamia kwenye ajali ya ndege katika eneo la Mwihoko kaunti ya Kiambu walikuwa wakielekea katika eneo la Hergeisa nchini Somalia kumwokoa mtoto aliyekuwa katika hali mbaya.
Haya ni kwa mujibu wa shirika la utafiti wa matibabu barani Afrika AMREF, ambalo limethibitisha kuwa waathiriwa walikuwa madaktari wake.
Afisa mkuu wa mtendaji wa shirika hilo Stephen Gitau, amesema mtoto huyo alihitaji msaada wa dharura.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































