COMOROS KWENYE UKINGO WA HISTORIA, STARS WAZIMWA
Katika mashindano ya kufuzu kwa Kombe la Dunia la soka mwaka wa 2026, timu ya taifa ya Morocco ndio timu pekee kati ya 9 zinazotarajiwa kufuzu barani Afrika, ambayo imefuzu kushiriki mashinadano hayo huku ikifuatiwa kwa ukaribu na timu ya Misri.
Comoros nao hapo jana wameongeza matumaini yao ya kushiriki mashindano ya kombe hilo kwa mara ya kwanza mwaka ujao baada ya kuwatandika Central Africa Republic mabao 2-0 na sasa wanashikilia nafasi ya 2 katika kundi I kwa alama 15, Black Stars wa Ghana wakiwa mbele kwa alama 1 pekee.
Mashindano hayo yaliyotarajiwa kuhusisha nchi 54 katika vikundi 9, sasa inahusisha nchi 53 baada ya timu ya taifa ya Eritrea kujiondoa kwenye orodha ya washindani.
Kila mshindi katika kila kundi atashiriki moja kwa moja katika kombe kuu, huku wengine watakaofuata wanne watashiriki mashindano ya mchujo katika nusu fainali na kisha wataofaulu kushinda katika fainali watashiriki mashindano ya mchujo ya shirikisho ya kimataifa maarufu kama inter-confederation playoff.
Wakati uo huo, timu ya taifa ya Soka Hrambee Stars inajiandaa kwa mechi yake dhidi ya Seychelles hapo kesho, baada ya matumaini yake ya kufuzu kwenye kombe hilo kuzimwa Ijumaa wiki jana kufuatia kichapo cha mabao 3:1 mikonnoni mwa the Gambia wanaonolewa na aliyekuwa kocha mkuu wa klabu ya Gor Mahia Jonathan McKinstry.
Dimba hilo la mwaka ujao litaandaliwa katika miji 16 ya mataifa matatu ya Mexico, Canada na Marekani mwaka ujao.
Imetayarishwa na Nelson Andati
English 


























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































