TUKO TAYARI KWA MADAGASCAR
Kocha Mkuu Benni McCarthy amesema harambee Stars iko tayari kwa mtihani mgumu kutoka kwa Madagascar kesho, lakini Madagascar inapaswa kutarajia uzoefu mgumu zaidi kutoka kwa Kenya.
Katika kikao chake na wanahabari leo kabla ya mchuano wa robo fainali katika uwanja wa MISC Kasarani, McCarthy alizungumza kwa heshima kuhusu Madagaska, lakini akaonya kuwa ana fomula ya kuwachapa.
Nahodha Msaidizi Daniel Sakari aliunga mkono hisia za makocha wake.
Madagascar ilijikatia tiketi ya kucheza na Harambee Stars baada ya kumaliza nafasi ya pili katika Kundi B nyuma ya Tanzania, huku Kenya ikimaliza kileleni mwa Kundi A.
Pambano hilo litaanza kesho 5pm, huku mashabiki 27,000 pekee wakiruhusiwa kuingia uwanjani
Imetayarishwa na Nelson Andati
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































