#Local News

BARCHOK APATA PIGO MAHAKAMANI

Gavana wa Bomet Hillary Barchok amepata pigo baada ya mahakama kutupilia mbali ombi lake la kuitaka itoe amri inayozuia kukamatwa au kushtakiwa kwake kuhusiana na tuhuma za ufisadi zinazomwandama.

Akitoa uamuzi wake, jaji wa mahakama kuu Bahati Mwamuye ameamuru kesi hiyo isikilizwe wiki ijayo.

Kulingana na gavana huyo ambaye alikuwa ameagizwa kujiwasilisha mbele ya tume ya maadili na kukabili ufisadi EACC, mashtaka ya DPP yanelnga kumchafulia jina na yasiyo na msingi.

Wakati uo huo, EACC inatarajiwa kutoa mwelekeo kuhusu mashtaka ya ufisadi yanayomkabili aliyekuwa gavana wa Bungoma Wycliffe Wangamati, ambaye amehojiwa na tume hiyo hii leo.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

BARCHOK APATA PIGO MAHAKAMANI

AFISA WA KENYA AUAWA HAITI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *