IEBC YATANGAZA TAREHE YA CHAGUZI NDOGO
Maandalizi ya chaguzi ndogo 23 nchini yameshika kasi huku tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC ikitangaza mikakati ya kuzifanikisha, katika juhudi za kuhakikisha uwazi kwenye uchaguzi huo.
Mwenyekiti wa tume hiyo Erastus Ethekon ametangaza kuwa chaguzi hizo zitaandaliwa tarehe 27 mwezi Novemba mwaka huu, huku kampeni zikiratibiwa kuanza tarehe 8 mwezi ujao, siku ambayo pia wawwaniaji watawasilisha vyeti vyao kwa wasimamizi wa uchaguzi.
Miongoni mwa maeneo ya chaguzi ndogo ni wadhifa wa useneta katika kaunti ya Baringo, maeneo bunge la Malava, Ugunja, Kasipul, Banisa, Magarini na Mbeere North.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 


























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































