#Local News

FAHARI YA KENYA JAPAN, ULIMWENGUNI

Kenya inaendelea kusherehekea ushindi wa mwanariadha Faith Kipeygon aliyeishindia nchi nishani ya dhahabu hapo jana katika mbio za mita 1,500 kwenye mashindano ya ubingwa wa dunia jijini Tokyo Japan.

Kipyegon ambaye sasa ameshinda ubingwa huo mara 4, alimwongoza mkenya mwenzake Dorcus Ewoi aliyemaliza katika nafasi ya 2 na hivyo kufikisha jumla ya medali 5 kwa taifa katika mashindano hayo yanayoendelea.

Kipyegon alikamilisha mbio hizo katika muda wa dakika 3 sec 52.15 na kushinda dhahabu ya 4, na hivyo kufikia rekodi ya raia wa Morocco Hisham El Guerrouj ya dhahbu 4 katika mbio za wastani.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

FAHARI YA KENYA JAPAN, ULIMWENGUNI

USAJILI WA MAKURUTU WA POLISI KUANZA

SHA IMEVUNJA REKODI YA NHIF, MWANGANGI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *