#Local News

WAHADHIRI WALAUMU VYUO VIKUU KWA MGOMO

Mgomo wa wahadhiri wa vyuo vikuu vya umma umeendelea kutatiza masomo kwa wiki ya pili sasa licha ya serikali kuonya kuwachukulia hatua za kinidhamu wahadhiri walio kwenye mgomo ambao serikali inasema ulifutiliwa mbali na mahakama.

Katika chuo kikuu cha Dedan Kimathi, wahadhiri chuoni humo wamedai kukandamizwa na usimamizi wa chuo hicho, wakisema umekataa kuwapa haki yao licha ya serikali kutuma shilingi milioni 44 kama sehemu ya makubaliano ya kusitisha mgomo.

Muungano wa UASU tawi la chuo hicho sasa umeitaka tume ya EACC na wizara ya elimu kuingilia kati.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

WAHADHIRI WALAUMU VYUO VIKUU KWA MGOMO

ODM YAMTEUA MWANIAJI WA UBUNGE KASIPUL

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *