WANAOWALAGHAI WASANII MATATANI- SERIKALI
Serikali imeapa kuwalinda wasanii, wabunifu na wanamuziki dhidi ya walaghai wanaolenga kuwapunja, ikisema imeweka mikakati ya kuwakabili walaghai hao kikamilifu.
Kulingana na naibu rais Kithure Kindiki, serikali inalenga kuwaondoa watu binafsi ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakijinufaisha kwenye sekta hiyo huku wasanii wakiendelea kuteseka.
Alikuwa akizungumza na waimbaji zaidi ya 2000 nyumbani kwake kaunti ya Tharaka Nithi.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































