WAVINYA AKANA KUWA ‘KIZUIZI’ CHA MAENDELEO
Muungano wa magavana 3 kutoka kaunti za Ukambani umepuzilia mbali madai kwamba ndio wamekuwa wakiizuia serikali kuu kutekeleza miradi ya maendeleo eneo hilo.
Mwenyekiti wa muungano huo Wavinya Ndeti ambaye pia ni gavana wa Machakos, ameyataja madai hayo kuwa yasiyo na msingi, akisema waliwasilsha mapendekezo ya miradi kwa serikali kuu jinsi walivyotakiwa ila hadi sasa bado haijatekelezwa.
Wavinya alikuwa akizungumza katika eneo la Masinga.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 


























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































