#Local News

MARAIS WA ZAMANI WAJITOKEZA KWENYE UCHAGUZI WA MALAWI

Marais wawili wa zamani wa Malawi wamezindua kampeni za kuwania urais nchini humo, kwa lengo la kumandua rais wa sasa Lazarus Chakwera wanayesema amechangia kudorora wa uchumi wa taifa hilo.

Malawi kwa sasa inakabiliwa na mfumuko wa juu wa bei za bidhaa wa hadi asilimia 30, rais wa zamani Peter Mutharika mwenye umri wa miaka 85 akisema atatoa suluhu iwapo atachaguliwa kwenye uchaguzi mkuu wa tarehe 16 mwezi ujao.

Mwingine ni Joyce Banda, atakayewania kupitia chama cha People’s Party, aliyeongoza taifa hilo kati ya mwaka 2012 na 2014 kufuatia kifo cha rais wa wakati huo Bingu wa Mutharika, Banda alipokuwa akihudumu kama makamu wa rais.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

MARAIS WA ZAMANI WAJITOKEZA KWENYE UCHAGUZI WA MALAWI

WADAU WATAKA POLISI, FKF KUMAKINIKA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *