MAUAJI YA WAKILI YAIBUA MASWALI
Polisi jijini Nairobi wanachunguza mauaji ya kikatili ya wakili Kyalo Mbobu, aliyepigwa risasi na kuuawa papo hapo kwenye barabara ya Langa’ata na mtu aliyekuwa akitumia pikikipiki usiku wa kuamkia leo.
Walioshuhudia wanasema wakili huyo alikuwa pekee yake kwenye gari hilo, mauaji hayo yakikosolewa na chama cha wanasheria nchini LSK ambayo imeyataja kuwa tishio kwa utendakazi wa mawakili.
Mbobu mwenye tajriba ya zaidi ya miaka 29 kama wakili, aliwahi kuhudumu kama naibu mwenyekiti wa jopokazi la kutatua mizozo ya vyama vya kisiasa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 










































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































