WAWAKILISHI WADI WA GUSII IKULU
Rais William Ruto anatarajiwa kuongoza kikao na wawakilishi wadi kutoka kaunti za eneo la Gusii ambazo ni Kisii na Nyamira, wakiongozwa na gavana Simba Arati kabla ya kuanza ziara yake katika eneo hilo.
Mabunge ya kaunti hizo tayari yamesitisha vikao vyake ili kuwaruhusu wawakilishi wadi hao kuhudhuria kikao cha rais katika Ikulu ya Nairobi, huku wakijitetea dhidi ya ukosoaji kwamba wametelekeza majukumu yao muhimu ya bunge ili kuhuduria kikao hicho.
Hadi sasa, gavana wa Nyamira Amos Nyaribo ambaye ni mwandani wa Waziri wa zamani Fred Matiang’i, hajabainika iwapo atahudhuria au la.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































