WANAJESHI WAKOSESHA UTULIVU MANDERA
Utata kuhusu kuwepo kwa vikosi vya jeshi la Jubaland katika kaunti ya Mandera umeendelea kuibua mijadala nchini huku serikali ikikana kuwepo kwa vikosi hivyo.
Kulingana na wakazi wa eneo la mpaka la Border One kwenye kaunti hiyo, shughuli za kila siku ikiwemo masomo zimetatizika kutokana na uwepo wa vikosi hivyo, hatua iliyowalazimu kufanya maandamano hapo jana kuishinikiza serikali kuviondoa vikosi hivyo.
Hata hivyo, Waziri wa usalama Kipchumba Murkomen amesema hakuna jeshi la Jubaland nchini, huku aliyekuwa naibu rais Rigathi Gachagua akiikosoa serikali kwa madai ya kuwapuuza wakazi wa Mandera.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































