MAGAVANA WAENDELEA KUMULIKWA
Magavana zaidi nchini wameendelea kujipata chini ya darubini ya vyombo vya uchunguzi kuhusiana na sakata za ufisadi katika kaunti zao, wa hivi punde akiwa gavana wa Nakuru Susan Kihika.
Akiwa mbele ya kamati ya uhasibu katika bunge la seneti hapo jana, Kihika alikuwa na wakati mgumu kueleza madai ya ufujaji wa zaidi ya shilingi milioni 22 kupitia miradi iliyokwama, kikiwemo choo cha shilingi milioni 1 ambacho ujenzi wake haujakamilika.
Kamati hiyo imeitaka tume ya maadili na kukabili ufsiadi EACC kumchunguza.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 


























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































