FAMILIA YA AFISA ALIYEFARIKI HAITI YAOMBOLEZA
Familia ya afisa wa polisi aliyefariki kwenye ajali nchini Haiti Kennedy Mutuku imetoa wito kwa serikali kuisaidia katika kuurejesha nchini mwili wa afisa huyo ili kufanikisha mazishi nyumbani kwao katika kaunti ya Machakos.
Kulingana na Sera Ndung’e ambaye ni mamake Mutuku, kifo cha mwanawe wa pekee kimesababisha pigo kwa familia, akisema mwanawe alikuwa amepanga kuwatembelea mwezi Novemba wakati wa likizo yake.
Mutuku alikuwa miongoni mwa maafisa 8 wa polisi waliojeruhiwa kwenye ajali wakati gari walimokuwa lilipata ajali.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































