#Local News

WAKUU WA MBUGA YA NAKURU MAHAKAMANI

Mahakama jijini Nakuru imewaagiza maafisa wawili wakuu wa mbuga ya Wanyama ya Ziwa Nakuru kufika mahakamani kuhusiana na utekaji nyara wa mvuvi Brian Odhiambo, baada ya mashahidi wawili hapo jana kutoa kauli za kukanganya kuhusiana na tukio hilo.

Kwenye vikao vya kusikiliza kesi hiyo, mashahidi 2 waliiambia mahakama kwamba waliwaona maafisa wa idara ya huduma kwa wanyamapori KWS wakimkamata na kumtesa Odhiambo ambaye ametoweka tangu Januari mwaka huu.

 Maafisa hao watafika mahakamani Jumatatu wiki ijayo.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

WAKUU WA MBUGA YA NAKURU MAHAKAMANI

WAHADHIRI MOI WAENDELEA NA MGOMO

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *