#Sports

KIKOSI CHA MAGONGO CHAZINDULIWA

Muungano wa Mpira wa Magongo wa Kenya umezindua kikosi kinachoongoza kitakachowakilisha nchi katika mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika yatakayoandaliwa Ismailia, Misri, kuanzia Oktoba 11 hadi 18, 2025.

Akizungumza katika kikao na wanahabari katika Uwanja wa City Park jijini Nairobi, rais wa Muungano wa Mpira wa Magongo wa Kenya, Nahashon Randiek, alithibitisha wachezaji 18 waliochaguliwa kwa kila timu ya wanaume na wanawake.

Kocha huyo pia alisema kuwa timu hiyo inajumuisha mchanganyiko wa wanaume na wanawake wa wachezaji wenye uzoefu na kizazi kipya cha wanariadha, wakiwemo wachezaji kadhaa waliong’ara kwa Kenya kwenye michuano ya U21 nchini Namibia.

 Aliongeza kuwa mafunzo hayo yalikumbana na changamoto ambazo, kwa bahati nzuri, hazikuzuia maendeleo yake. Kwa matumaini kuwa hakuna changamoto zaidi, timu hizo zinatazamiwa kuondoka kati ya tarehe nane na tisa ya Oktoba.

Imetayarishwa na Nelson Andati

KIKOSI CHA MAGONGO CHAZINDULIWA

IMBENZI APIGIA UPATO KIKOSI CHAKE

KIKOSI CHA MAGONGO CHAZINDULIWA

CHELSEA WAZAMISHA BENFICA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *