WAPITA NJIA, BODA BODA 6 WAUAWA KERICHO-KISUMU
Watu 6 wamefariki papo hapo huku wengine 4 wakijeruhiwa baada ya kugongwa na lori katika soko la Kipsitet kwenye barabara ya Kericho kuelekea Kisumu usiku wa kuamkia leo.
Kamanda wa polisi kaunti ndogo ya Sigowet/Soin Lawrence Kisini amesema lori hilo lilikuwa likielekea upande wa Kisumu kabla ya kupoteza mwelekeo na kuwagonga wapita njia na wahudumu wa boda boda.
Mansura wamepelekwa kwenye hospitali ya rufaa mjini Kericho huku miili ikipelekwa kwenye hifadhi ya hospitali hiyo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 


























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































