OCHOLLA AFURAHISHWA NA KIKOSI CHAKE
Kocha Msaidizi wa KPA Samuel Ocholla amefurahishwa na juhudi na dhamira ya timu yake baada ya kupata ushindi wa mechi zote mbili wikendi katika Ligi Kuu ya Kikapu ya Wanawake nchini.
Siku ya Jumamosi, KPA iliishinda Strathmore Swords 73-51 na Jumapili wakaichapa ANU Panthers 83-39.
Ocholla alisisitiza kuwa timu hiyo itasalia na umakini kwani sasa ipo kileleni mwa msimamo wa ligi ikiwa na pointi 41 katika michezo 21, ikishinda 20 na kupoteza mmoja.
Imetayarishwa na Nelson Andati
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































