#Sports

FKF YAOMBWA KUONGEZA MGAO WA PESA KWA LIGI KUU

shirikisho la Soka la Kenya (FKF) linafaa kuongeza zawadi ya pesa taslimu kwa mabingwa wa ligi ya nyumbani ili kuongeza ushindani wa vilabu vya Kenya katika ngazi ya bara.
Alisema kuwa Kushiriki katika mashindano ya CAF kunagharimu kati ya Ksh15 na Ksh20 milioni kwa mechi za nyumbani na ugenini na bila ya tuzo nzuri ya ya ndani kipesa, ni changamoto kubwa.
Hivi majuzi CAF ilitangaza marekebisho ya muundo wake wa kifedha, huku timu zinazoshiriki Ligi ya Mabingwa ya CAF na Kombe la Shirikisho sasa zikiwa na uhakika wa kima cha chini cha $100,000 (Ksh13 milioni) katika awamu ya awali, mara mbili ya zawadi ya $50,000 iliyoanzishwa mwaka jana.
Hii ina maana kwamba Polisi fc na washindi wa Kombe la FKF, Nairobi United, ambao watashiriki Kombe la Shirikisho la CAF, wote wamehakikishiwa kuimarika kifedha kuelekea hatua za bara.

Imetayarishwa na Nelson Andati

FKF YAOMBWA KUONGEZA MGAO WA PESA KWA LIGI KUU

HENDERSON AJIUNGA NA BRENTFORD

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *