RAIS RUTO AONYA WALAGHAI WA SHA WATAANDAMWA
Rais William Ruto amewaonya watu binafsi na hospitali dhidi ya kuilaghai mamlaka ya afya SHA, akisema kuwa wahusika watakamatwa na kufunguliwa mashtaka.
Katika kikao na wajumbe kutoka kaunti ya Kiambu katika Ikulu ya Nairobi, Ruto ameapa kuangamiza ulaghai wa aina yoyote katika bima ya SHA
Aidha, amezionya hospitali za umma dhidi ya kuwatoza wagonjwa ada zilizolipwa na serikali.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































