WABUNGE WAMENICHOSHA NA HONGO, RUTO
Rais William Ruto ameibua madai kwamba wabunge wamevuka mipaka katika kuitisha hongo wanapoichunguza serikali kuhusiana na masuala mbali mbali, akisema imemlazimu awaweke wazi.
Akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya ugatuzi katika kaunti ya Homa Bay, Rais amedai kuwa kamati za bunge zimekuwa zikiitisha hongo ili kuwasafisha maafisa wanaotuhumiwa katika Sakata mbali mbali.
Amesema ameiachia tume ya maadili na kukabili ufisadi kuchukua hatua.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 




















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































