HATUA ZAPIGWA KATIKA UCHUNGUZI WA MAUAJI NAIROBI
Polisi wamesema wamepata kanda muhimu za video kutoka maeneo kadhaa yakiwemo majengo ya kibinafsi zinazoonyesha hatua za mwisho za wakili aliyeuawa jijini Nairobi Kyalo Mbobu, ambazo wanasema zitasaidia katika uchunguzi wa mauaji hayo.
Kulingana na polisi, mwendazake alifanya mkutano kwa takribani saa 3 katika mkahawa mmoja kwenye barabara ya Milimani na watu ambao sasa wamejumuishwa kwenye uchunguzi, kabla yake kurejea afisini mwake majira ya saa 7 na dakika 45 za mchana.
Aidha, polisi wamesema mwendazake alikuwa akielekea nyumbani baada ya kuondoka afisini katika jumba la Chester House, akitumia barabara ya Wabera Street, City Hall Way, Parliament Road, Uhuru Highway kabla ya kuchukua barabara ya Lang’ata kupitia mzunguko wa Nyayo alipouawa baadaye mita chache kutoka makazi yake katika eneo la Boyani mtaani Karen.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































