UHAMISHO WA LIGI KUU YA UINGEREZA
Javi Guerra amekataa ofa ya kuongeza mkataba wake na Valencia, huku Manchester United ikisemekana kumfuatilia kiungo huyo wa kati wa Uhispania mwenye umri wa miaka 22.
Winga wa Manchester City na England Jack Grealish, 29, ni mmoja wa wachezaji kadhaa wa upande wa kushoto wanaofikiriwa na Napoli
Real Madrid wako tayari kutoa pauni milioni 100 kwa kiungo wa kati wa Manchester City na Uhispania Rodri, 29.
Tottenham wanamfuatilia kwa karibu Kobbie Mainoo, huku kiungo huyo wa kati wa Manchester United akiwa bado hajakubali kuongezwa kwa mkataba wake kwa muda mrefu, ambao unamalizika 2027.
West Ham itachuana na Everton katika kinyang’anyiro cha kumnunua Douglas Luiz kutoka Juventus baada ya Aston Villa kujiondoa kwenye kinyang’anyiro cha kumnunua tena kiungo huyo wa kati wa Brazil mwenye umri wa miaka 27.
Atalanta inapanga kumnunua winga wa Liverpool na Italia Federico Chiesa, 27, ikiwa Juventus itafikia thamani ya €50m (£43m) ili kumsajili fowadi wa Nigeria Ademola Lookman, 27.
West Ham wako kwenye mazungumzo na Callum Wilson kuhusu uhamisho wa bila malipo kufuatia mshambuliaji huyo wa Uingereza mwenye umri wa miaka 33 kuachiliwa kutoka Newcastle.
Spurs wanafuatilia hali ya kandarasi ya Joao Palhinha wa Bayern Munich. Klabu hiyo ya Bavaria iko tayari kufanya mazungumzo iwapo ofa itawasili kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ureno mwenye umri wa miaka 30. (Florian Plettenberg), nje
RB Leipzig wamemtaja kiungo mshambuliaji Xavi Simons katika kikosi chao cha kambi ya mazoezi, licha ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 kuhusishwa na kuhamia Chelsea na mchezaji huyo wa kimataifa wa Uholanzi kufanya mazungumzo kuhusu masuala ya kibinafsi na The Blues.
Borussia Dortmund wana nia ya kumsajili kiungo wa kati wa Brighton mwenye umri wa miaka 20 Facundo Buonanotte. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina alikaa kwa mkopo Leicester City msimu uliopita na amebakiza miaka mitatu kwenye mkataba wake.
Mazungumzo kati ya Marseille na Feyenoord kuhusu winga wa Brazil Igor Paixao yamesimama baada ya dau la klabu hiyo ya Ufaransa la pauni milioni 24 kutofikia bei iliyokuwa ikidaiwa.
Leeds United sasa wana matumaini ya kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25.
Kiungo wa kati wa Uturuki Hakan Calhanoglu amekuwa akihusishwa na kutaka kuondoka Inter Milan lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 anasema anataka kusalia katika klabu hiyo ya Italia.
Manchester City wanataka kumbakisha Ederson licha ya Galatasaray kuonyesha nia ya kumnunua mlinda mlango huyo wa Brazil mwenye umri wa miaka 31, ambaye anakaribia kuingia mwaka wa mwisho wa mkataba wake.
Fulham wana uhakika wa kumbakisha kiungo wa kati wa akademi Seth Ridgeon licha ya Manchester United, Liverpool na Chelsea kuonyesha nia ya kumnunua nahodha huyo wa vijana wa chini ya miaka 17 wa England.
Imetayarishwa na Nelson Andati
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































