#Business

DENI LA KENYA LINALIPA MISHAHARA SI MAENDELEO, DATA YA HAZINA YAFICHUA

Sehemu kubwa ya fedha zilizokopwa za Kenya zilizotengwa kwa miradi ya maendeleo imeshuka hadi kiwango cha chini kabisa katika kipindi cha mwongo mmoja, na hivyo kufichua ongezeko la matumizi ya deni ili kulipia gharama za kawaida kama vile mishahara na pensheni.

Takwimu za Hazina ya fedha zinaonyesha kuwa katika mwaka wa fedha wa 2024-2025, shilingi bilioni 582.9 ambayo ni asilimia 56.4 zilitumika kwa maendeleo, huku shilingi bilioni 451.3 sawa na asilimia 43.6 zikielekezwa kwa matumizi ya kawaida.

Hii ni kinyume na sheria ya usimamizi wa fedha za umma, ambayo inaamuru kwamba fedha za mkopo zitumike kwa maendeleo pekee. Mwaka uliotangulia kulishuhudiwa kiwango cha chini cha asilimia 33.2 ya fedha zilizokopwa zikizotumika kwa matumizi ya kawaida.

Mabadiliko hayo yanatokana na matumizi duni ya fedha za maendeleo na kuongezeka kwa ukopaji wa ndani. Tangu 2017, serikali imekiuka sheria za kukopa mara kwa mara, huku matumizi ya maendeleo yakiendelea kupungua.

Imetayarishwa na Maurine Amwayi

DENI LA KENYA LINALIPA MISHAHARA SI MAENDELEO, DATA YA HAZINA YAFICHUA

CHELSEA WAZAMISHA LINCOLN

DENI LA KENYA LINALIPA MISHAHARA SI MAENDELEO, DATA YA HAZINA YAFICHUA

WAHADHIRI WALAUMU VYUO VIKUU KWA MGOMO

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *