#Local News

MCAS BUNGOMA WACHUNGUZWA NA EACC

Waakilishi wadi 6 kaunti ya Bungoma wanachunguzwa na maafisa wa tume ya maadili na kupambana na ufisadi Eacc kwa madai ya kujihusisha na biashara na kaunti kinyume na sheria.

Wahusika wanadaiwa kutumia kampuni zinazomilikiwa na jamaa na wandani wao kuchukua tenda za miradi ya ujenzi zinazogharimu mamilioni ya fedha.

Zaidi ya shilingi milioni 140 zinadaiwa kulipwa kwa miradi hiyo ambayo haijamalizika iliyo kwenye wadi zao.

Imetayarishwa na Maureen Mukhobe

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *